Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi 10,000 kutoka Syria wakimbilia Uturuki

Wakimbizi 10,000 kutoka Syria wakimbilia Uturuki

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kwa sasa zaidi ya wakimbizi 10,000 kutoka Syria wamepewa hifadhi na serikali ya Uturuki kwenye kambi nne kati ya ya mpaka kati ya nchi hizo mbili.

 Tangu Juni 7 kati ya wakimbizi 500 na 1000 wamekuwa wakiingia nchini Uturuki kila siku. UNHCR inasema kuwa ilijumuika kwenye ziara iliyoandaliwa na serikali ya uturuki kwenda mji wa Jisr Al Shugour ambapo iligundua kuwa huenda watu wengi wamehama kufuatia idadi ndogo ya watu walio kwenye mji huo

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

UNHCR inasema kuwa jitihadi na serikali ya Syra za kuwahakikishia usalama, na makao wakimbizi kutoka Syria ni za kupewa sifa lakini hata hivyo kuna wasi wasi kuhusu hatma ya akina mama na watoto wanaochukua zaidi ya asilimia 50 ya idadi yote ya wakimbizi hao.