ICC inachunguza madai ya kutumia madawa ya ngono kwa ubakaji

9 Juni 2011

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC inachunguza endapo kiongozi wa Libya Muammar Qadhafi aliwapa askari wanaume dawa za kuongeza nguvu za kiume ili wawabake wanawake.

Luis Moreno Ocampo amesema ubakaji umekuwa ukitumika kama silaha ya vita katika baadhi ya migogoro ili kuwaadhibu na kuwanyanyasa wanawake na ofisi yake inakusanya ushahidfi wa madai hayo Libya.

Ocampo amesema tumebaini baadhi ya vitu kuthibitisha suala la matumizi ya Viagra inaonyesha kwenye sera. Walikuwa wananunua makontena yaliyosheheni dawa hizo ili kuwezesha ubakaji wa wanawake na kuna uwezekano wa kupata taarifa zaidi kuthibitisha sera hiyo.

Bwana Ocampo amesema mashitaka mapya ya ubakaji wa kundi la watu yanaweza kufunguliwa dhidi ya Kanali Qadhafi mara baada ta kutathimini ushahidi mpya.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter