Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bragg ataoa wito kwa misaada zaidi kwenye maeneo ya vijiji nchini DRC

Bragg ataoa wito kwa misaada zaidi kwenye maeneo ya vijiji nchini DRC

Naibu mratibu wa huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa Catherine Bragg amesema kuwa mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na washirika wao wanastahili kupeleka misaada zaidi katika maeneo yaliyo mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Akiongea baada ya kukamilisha ziara ya siku tano nchini DRC ambapo alikutana na maafisa wa serikali , walinda amani wa Umoja wa Mataifa , watoa misaada na raia wa DRC waliokimbia makwao bi Bragg amesema kuwa waliokimbia makwao mashariki na kaskazini mashariki mwa DRC wanayaogopa makundi yaliyojihami yanayoendeleza uovu ukiwemo mauaji na ubakaji. Bi Bragg alizuru mji wa Dungu ulio kaskazini mashariki mwa DRC ambapo maelfu ya watu wanaishi kwenye kambi.