Marekani imerejea wito kwa Syria kuruhusu wachunguzi wa kimataifa

31 Mei 2011

Mbinyo umeendelea kutolewa kwa serikali ya Syria inayotakiwa kufungua milango ili kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini humo kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa uharibifu wa haki za binadamu.

Akizungumza kwenye mkutano wa baraza la haki za binadamu mjini Geneva, balozi wa Marekani Eileen Donahue amesisitiza kuwa mamlaka za Syria zinapaswa kuwaruhusu wachunguzi hao kwani huu ni wakati muafaka wa timu ya wataalamu kuingia nchini humo kuendesha uchunguzi huru juu ya masuala yanayohusu uvunjifu wa haki za binadamu.

Amesema kuwa tayari kamishna hiyo ya uchunguzi imekubaliwa kufanya kazi zake nchini Libya, lakini jambo la kushangaza ni kuwa serikali ya Syria bado imeendelea kuweka ngumu juu ya hatua ya kukaribishwa wataalamu hao.

Mwanadiplomasia huyo pia amelitaka baraza hilo la haki za binadamu kuinyoshea kidole serikali ya Syria isitishe videndo vyake vya uvunjivu wa haki za binadamu ikiwemo mauwaji, kuwaweka korokoroni waandamanaji.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud