Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi Afrika wataka uchunguzi wa vifo vya wahamiaji

Viongozi Afrika wataka uchunguzi wa vifo vya wahamiaji

Viongozi barani Afrika wanatoa wito wa kutaka kufanyika uchunguzi kuhusu madai ya kutelekezwa kwa wahamiaji kaskazini mwa Afrika. Hii ni kulingana na balozi Ositadinma Anaedu kutoka Nigeria alipohutubia mkutano wa baraza la haki za binadamu mjini Geneva.

Balozi huyo amesema kuwa ujumbe kutoka Afrika una wasi wasi mkubwa kuhusu hali ya wahamiaji akiongeza kuwa wanayopitia wahamiaji hao kwenye mipaka ya ulaya yakiwemo kukataliwa na kufungwa hayashutumiwi.

Kulingana na makubaliano ya Umoja wa Mataifa na yale ya haki za binadamu ni kuwa wahamiaji wanastahili kuhudumiwa kwa njia nzuri