Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen iko katika hatihati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe

Yemen iko katika hatihati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe

 

Kumekuwa na ongezeko la machafuko ya hatari nchini yemen katika siku chache zilizopita ambayo yanaweza kulitumbukiza taifa hilo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu.

Idadi kamili ya raia waliokufa ni vigumu kupata ingawa wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo wanataja kuwa zaidi ya watu 860 wameuawa wakiwemo wanawake na watoto.

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema anatiwa hofu na machafuko na kushambuliwa kwa waandamanaji, pia makombora yanayorushwa na majeshi ya serikali kwenye makazi ya raia. Rupert Colvile ni msemaji wa kamishina mkuu wa haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Kamishina mkuu amesema timu ya wachunguzi wa haki za binadamu watazuru Yemen mwezi Juni kwa mwaliko wa serikali ili kutathimini hali ya haki za binadamu katika nchi hiyo.