Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yashughulikia dhuluma za kimapenzi kwenye kambi nchini Haiti

IOM yashughulikia dhuluma za kimapenzi kwenye kambi nchini Haiti

Akina mama na wasichana wa umri mdogo wanaoishi kwenye kambi nchini Haiti baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba nchi hiyo mwaka uliopita ni kati ya wale waliopitia dhulum za kimapenzi zinazohusiana na ghasia. Kulingana na takwimu kutoka kwa polisi na vituo vya kiafya pamoja na mashirika ya kimataifa zinaonyesha kuwa kuripotiwa kwa visa vingi vya dhuluma za kimapenzi kumetokana na uaminifu kati ya polisi na waathiriwa. Hata kama hakujakuwa na utafiti rasmi kubaini kuongezeka kwa visa hivyo nchini Haiti kuna takwimu kuhusu suala hilo. Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anaeleza.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)