Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa ICC kumshitaki Gaddafi na watu wengine wawili Libya

Mkuu wa ICC kumshitaki Gaddafi na watu wengine wawili Libya

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Luis Moreno Ocampo leo ametangaza kufungua mashitaka na kutaka hati ya kukamatwa Rais wa Libya kanali Muammar Gaddafi, mtoto wake wa kiume Saif al-Islam na mkuu wa upelelezi Abdullah al-Sanussi kwa kupanga na kufanya mashambulizi dhidi ya raia.

Ocampo amesema mashambulizi ya kupangwa yametapakaa nchini Libya na majaji wa ICC wataamua endapo kuna sababu za msingi za kutoa hati ya kukamatwa watu hao ama la. Ocampo amesema mashambulizi hayo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

(SAUTI YA LUIS MORENO OCAMPO)

Kufuatia tamko hilo serikali ya Libya imesema itapuuza hatua hiyo. Naibu waziri wa mambo ya nje Khalid Kaim amesema mahakama hiyo na shughuli zake zinatia shaka, na kwamba serikali ya Libya haiitambui kama ilivyo nchi nyingi za Afrika na Marekani, na Libya itapuuza tangazo lolote la mahakama hiyo.