Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakenya waliotekwa nyara na maharamia kuachiliwa huru

Wakenya waliotekwa nyara na maharamia kuachiliwa huru

Mabaharia 43 waliotekwa nyara wakiwa ndani ya meli ya uvuvi na kuzuiliwa na maharamia wa Kisomali tangu Oktoba mwaka jana -wa 2010, hatimaye wamerejea nyumbani Kenya na kupokelewa kwa furaha na jamaa zao, baada ya kuachiliwa huru wiki iliyopita.

Watu hao ni Wa-Kenya 39 pamoja na raia WANNE wa Korea, waliotekwa nyara wakivua samaki karibu na Somalia. Walikuwa katika meli inayomilikiwa na kampuni moja ya Korea.

Meli iliyowabeba MV Golden Wave imetia nanga leo (Jumanne ) katika bandari ya Mombasa, ambapo kwenye mahojiano na waandishi wa habari, mabaharia hao wamedokeza kuwa walilazimishwa kujiunga na wasomali na kuziteka nyara meli zingine, kama njia moja ya kujikomboa.

Mwandishi wa Habari Josephat Kioko wa Mombasa alikuwa miongoni mwa watu katika bandari wakati meli hiyo ilipotia nanga, na ametuma ripoti ifuatayo.