Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa UM Nepal UNMIN umefungwa rasmi

Mpango wa UM Nepal UNMIN umefungwa rasmi

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini , UNMIN, unamalizika kwa mkuu wa mpango huo kusema kwamba umetoa mchango mkubwa kwa mchakato wa amani wa nchi hiyo.

UNMIN ilianzishwa mwaka 2007 kuisaidia nchi hiyo iliyoko katika milima ya Himalaya katika kipindi cha mpito kuelekea amani ya kudumu baada ya muongo wa vita baina ya wanamgambo wanaofuata siasa za Kimao dhidi ya utawala wa kifalme wa Nepal.

Utulivu wa kisiasa unaendelea lakini kama anavyosema mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo abaye ndiye mkuu wa UNMIN Karin Landgren mpango huo umeleta mabadiliko. Anasema ingawa mchakato bado haujakamilika mpango wa Umoja wa Mataifa , umetimiza wajibu wake na nina imani umetoa mchango mkubwa katika mchakato wa amani.

Umma wa Nepal umekuwa na matarajio makubwa kwa mpango huo, na wamejitahidi kuyatimiza, na sasa mpango unaondoka mtafaruku uliosalia wa kisiasa unaweza tu kutatuliwa na pande husika nchini humo.