Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkakati kabambe umewekwa na serikali ya mpito kuinusuru Somalia:Mahiga

Mkakati kabambe umewekwa na serikali ya mpito kuinusuru Somalia:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amefanya ziara ya ghafla Moghadishu Somalia.

Akiwa nchini humo amekutana na Rais Sheikh Sharifu Ahmed na waziri mkuu wa nchi hiyo. wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo usalama, tatizo la ukame, misaada na ulinzi, lakini kikubwa zaidi ni mkakati mpya uliowekwa na serikali ya Somalia kumaliza uasi nchini humo na kuleta amani ya kudumua baada ya zaidi ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Je ni mkakati gani huo tegea sikio mahojiano haya kati ya mkuu wa Idhaa ya redio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha na Balozi Mahiga anayeanza kwa kufafania kwa nini kaenda Somalia ghafla.