Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupuuza "Holocaust" ni kuwadhihaki wayahudi

Kupuuza "Holocaust" ni kuwadhihaki wayahudi

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa kupuuza mauwaji ya Holocaust ni sawa na kukaribisha hasira na chuki kwa jamii ya wayahudi.

Kiyo Akasaka amesema kuwa kwa yoyote anayekana kwamba hakukutokea mauji hayo ni kitendo cha kuwasarisha jamii ya Wayahudi ambao walikubwa na vitendo hivyo vya kikatili.

Akizungumza kwenye kongamano moja linaloangazia hali ya historia na hali ya mambo ya sasa, Kiyo Akasaka amewaambia wajumbe kwenye kongamano hilo linalofanyika huko Dublin, Ireland kuwa lazima kuyakataa mawazo yanayotaka kupindisha ukweli wa mambo.

Amewataka wajumbe hao kutobwete badala yake kuongeza juhudi ili kurekebisha hadithi za kufikirika zinazotolewa na wachache wenye nia ya kutaka kupindisha ukweli wa mambo juu ya mauwaji ya Holocaust