Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India yastahili kuwa mjumbe wa kudumu baraza la usalama:Rice

India yastahili kuwa mjumbe wa kudumu baraza la usalama:Rice

Marekani inaunga mkono hoja ya kupanua wigo wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuongeza idadi ya wajumbe wa kudumu na wasio wa kudumu.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema miongoni mwa wajumbe inaowataka waongezwe ni pamoja na India. Nchi zinazoendelea zinataka kuwepo na mabadiliko kwenye baraza la usalama ya kujumuisha wajumbe wa kudumu kutoka kanda zote na kumaliza miongo ya utawala wa wajumbe watano tuu wa kudumu kwenye baraza hilo.

Akizungumza wakati wa mjadala wa baraza la usalama kuhusu suala hilo balozi Rice amerejea mtazamo wa Rais Obama alioutoa mapema wiki hii alipozuru India.Bi rice amesema "Tamko la Rais la kuunga mkono India kwenye uanachama wa kudumu wa baraza lianaonyesha ukweli kwamba bila shaka demokrasia kubwa ya India inatoa mchango wa maana kwa amani na usalama wa dunia na ni vikumu kupokea mabadiliko ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakalojumuisha wajumbe wapya bila India kama mjumbe wa kudumu.