Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yazitaka nchi za G-20 kuzuia uchafuzi wa mazingira

UNEP yazitaka nchi za G-20 kuzuia uchafuzi wa mazingira

Wakati viongozi wa dunia wanapokusanyika mjini Seoul nchini Korea Kusini kwenye mkutano wa nchi zilizostawi na zile zinazoinukia kiuchumi za G20, mkurugenzi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Achin Steiner ametoa wito kwa viongozi hao kutumia ahadi zao za awali katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na pia katika kujikwamua kutoka kwa hali mbaya ya uchumi.

Steiner alipongeza hatua za mataifa ya G20 za kuyainua mabenki na kukabiliana na hali mbaya ya kiuchumi iliyoikumba dunia lakini akaongeza kuwa masuala kama vile upatikanaji wa nafasi za ajira na kupunguza umaskini katika karne hii ya 21 havitafanyika kwa njia iliyo rahisi.

Steiner ameipongeza Korea Kusini ambaye ni mwandalizi wa mkutano huo kwa hatua ilizo piga kuwekeza katika teknolojia isiyochafua mazingira na katika sekta zinazopunguza uchafuzi wa mazingira