Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM atilia shaka mwenendo wa uhuru wa kujieleza Panama, baada ya waandishi kuhukumiwa

Mjumbe wa UM atilia shaka mwenendo wa uhuru wa kujieleza Panama, baada ya waandishi kuhukumiwa

Mjumbe wa jopo huru la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza Frank La Rue ameelezea masikitiko yake kufutiwa kufungwa kwa waandishi wa habari 2 wa Panama ambao walitiwa hatiana baada ya kukutikana na kosa la kimazingira.

Waandishi hao pia walipigwa marafuku kwa kipindi cha mwaka mmoja kutofanya kazi yoyote ya uandishi wa habari.

Bwana La Rue amesema kuwa uamuzi huo wa mahakama unazidisha hali ya wasiwasi hasa panapohusika uhuru wa raia kupata habari kuhusiana na mwenendo wa ofisi za umma.

Licha kwamba hukumu hiyo inaweza kubadilishwa na waandishi hao kulazimishwa kulipa faini lakini hata hivyo mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa anaona kwamba vitendo kama hivyo vinarudisha nyuma juhudi za kuleta uhuru wa maioni na kujieleza.