Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya Cambodia ni muhimu kukabiliana na uhalifu dhidi ya ubinadamu:Ban

Mahakama ya Cambodia ni muhimu kukabiliana na uhalifu dhidi ya ubinadamu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko katika ziara ya siku mbili nchini Camboadia na kuzungumzia mambo mbalimbali.

Akiwa nchini humo amekutana na maafisa wa ngazi za juu wa serikali akiwemo waziri mkuu Hun Sen ambaye wamejadili naye masuala mbalimbali ya kitaifa na kikanda, na suala la mahakama inayoshughulikia uhalifu wa utawala wa Khmer Rouge inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.  Ban amesema Umoja wa Mataifa unaendelea na msimamo wa kuiunga mkono mahakama hiyo, na kugusia umuhimu wa haja ya kuwachukulia hatua waliohusika na uhalifu wa kutisha katika miaka ya 1970.

Ban amesema kuwafikisha mahakamani maafisa wa Khmer Rouge hata kama ni miaka 30 baadaye ni ujumbe mzito kwa watenda uhalifu, ujumbe kwamba ukwepaji wa sheria hauvumiliki, iwe ni kwa watu wa Cambodia na serikali yao ,Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.

Ban na waziri mkuu wamejadili pia suala la Myanmar hasa uchaguzi mkuu unaotarajiwa Novemba 7 na kusema Umoja waMataifa utaendelea kuwasaidia watu wa Myanmar.