Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathirika wa mafuriko Pakistan wasipuuzwe:UM

Waathirika wa mafuriko Pakistan wasipuuzwe:UM

Kamati tatu za Umoja wa Mataifa zinazohusika na masuala ya haki za binadamu zinataka waathirika wa mafuriko nchini Pakistan wasisahaulike.

Kwa pamoja zimetoa wito kwa utawala wa Pakistan na mashirika mengine ya kutoa misaada kuzingatia haki wakati wa kutoa misaada ili kuzuia kuteseka kwa waathirika wa mafuriko nchini humo, mafuriko yanayotajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kuikumba Pakistan kwa muda wa karne moja iliyopita. Jayson Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Kamati hizo zikiwemo za haki za watoto, kamati inayohusika na kubaguliwa kwa wanawake pamoja na inayohusika na haki za watu walio na ulemavu zinasema kuwa watu kutoka jamii ndogo , wakimbizi kutoka Afghanistan, wanawake , watoto na watu walio na ulemavu hususan wanaoishi sehemu za vijijini ndio walioathirika zaidi na mafuriko.

Takriban watu 1600 wameaga dunia nchini Pakistan na zaidi ya wengine 2000 kujeruhiwa kufuatia mafuriko hayo . Idadi ya watu walioathiriwa na mafuriko hayo moja kwa moja ni watu milioni 20 wakati zaidi ya nyumba milioni 1.9 zikiharibiwa.