Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 18 zateuliwa kujiunga na baraza la uchumi na jamii ECOSOC

Nchi 18 zateuliwa kujiunga na baraza la uchumi na jamii ECOSOC

Baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa limeteua nchi 18 kuwa wanachama wa baraza la Umoja wa Mataifa lililo na jukumu kushughulikia masuala ya kimataifa ya kiuchumi na kijamii ECOSOC.

Baraza hilo linalozijumuisha nchi 54 zinazoteuliwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa linakutana kila mwaka kujadili masuala yanayohusiana na ushirikiano wa kiuchumi na kijamii pamoja na maendeleo. Nchi hizo ni Australia, Cameroon, China, Ecuador, Finland, Gabon, Hungary, Latvia, Malawi, Mexico, Nicaragua, Norway, Pakistan, Qatar, Jamhuri ya Korea, Urusi, Senegal na Uingereza .

Kati ya masuala yanayojadiliwa kwenye mikutano ya ECOSOC ni kama vile malengo ya milennia,ushirikiano wa kimaendeleo wa kimataifa na hali ya uchumi duniani. Mkutano wa ECOSOC mwaka huu uliangazia masuala ya ushirikiano wa kimaendelea ,usawa wa kijinsia na kuwainua wanawake na hali ya uchumi duniani.