Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wengi wameachwa nje kwenye uchaguzi nchini Myanmar:UM

Wengi wameachwa nje kwenye uchaguzi nchini Myanmar:UM

Mjumbe maalum kuhusu haki za binadamu nchini Myanmar ameutaka utawala wa nchi hiyo kuwaachilia wafungwa wote wenye dhamiri akiwemo Aung San suu Kyi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi uliotishwa na serikali mwezi ujao.

Akilihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa Tomas Ojea Quintana amesema kuwa watu hawa wote wakiwemo viongozi wa wanafunzi , wanachama wa vyama, viongozi wa jamii ndogo ndogo na wale waliofungwa kwa kutekeleza haki ya kutoa maoni yao au kukutana na wengine wana wajibu wa kutekeleza kwenye uchaguzi huu wa kihistoria.

Quintana ameliambia baraza kuu kuwa kulingana hali ilivyo sasa ni vigumu kuandaliwa kwa uchaguzi ulio wa kweli nchini Myanmar na uwezekano wa uchaguzi huu kuleta mabadiliko kwa watu wa nchi hiyo bado ni jambo halijulikani.