Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki kwa watu wa jamii ndogo inaweza kuzuia mizozo:UM

Haki kwa watu wa jamii ndogo inaweza kuzuia mizozo:UM

Imebainika kuwa kuwanyima haki zao watu wa jamii ndogo ni moja ya sababu inayochochea kuwepo kwa mizozo.

Akiwasilisha ripoti mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa mtaalamu wa UM anayehusika na masuala ya jamii ndogo Gay McDougall amesema kuwa sababu kama hizo zinastahili kutatuliwa mapema ii kuzuia kutokea kwa mizozo.

Amesema kuwa kuruhusu jamii ndogo kupata haki zao zikiwemo za kisiasa na za kitamaduni kunaweza kuchangia kuwepo kwa utulivu wa kisiasa na wa kijamii. Kulingana na utafiti wa hivi majuzi ni kuwa zaidi ya asilimia 55 ya mzozo iliyotokea kati ya mwaka 2007 na 2009 ilitokana na ukiukaji wa haki za watu wa jamii ndogo.