Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama huru na zilizo dhabiti ndizo zinaweza kukabiliana na ghasia nchini Mexico: UM

Mahakama huru na zilizo dhabiti ndizo zinaweza kukabiliana na ghasia nchini Mexico: UM

Kutumika kwa sheria kwa njia inayofaa na viota dhidi ghasia nchini Mexico vitafanikiwa iwapo mahakama za nchi hiyo zitakuwa huru.

Akiwa kwenye ziara ya siku 15 nchini Mexico ambapo pia alikutana na Rais wa nchi hiyo Felipe Calderon Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za majaji na mawakili Gabriela Knaul amesema kuwa mabadiliko ya katiba ya mwaka 2008 kuhusu sheria za uhalifu ni hatua kubwa katika kutekelezwa kwa sheria. Lakini hata hivyo amesema kuwa mabadiliko hayo yanakabiliwa na vizingiti katika kutekelezwa kwake na inaonekana kutoungwa mkono kote nchini. Kwenye ziara yake mjumbe huyo alibaini kuwa wengi wa wananchi wa mexico hawapati haki ya kisheria hususan wale maskini , wanaoishi vijijini, wanawake na wahamiaji. Pia Knaul Alikutana na majaji wa mahakama kuu , makamishina wa tume za kutetea haki za binadamu ,wasomi na mashirika ya kimataia yasiyokuwa ya serikali.