Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanaojeruhiwa vitani Afghanistan ni kubwa mno:ICRC

Idadi ya wanaojeruhiwa vitani Afghanistan ni kubwa mno:ICRC

Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC inasema idadi ya majeruhi wa vita nchini Afghanistan imefikiwa idadi kubwa kabisa kuwahi kutokea.

Kwa mujibu wa ICRC majeruhi wanaopelekwa katika hospitali ya Mirwais kwa ajili ya matibabu ni kubwa mno na katika kipindi cha Agosti na Septemba mwaka huu majeruh waliofikishwa katika hospitali hiyo inayosaidiwa na ICRC ni mara mbili ya mwaka jana, kama anavyofafanua Christian Cardon msemaji wa ICRC nchini Afghanistan.

(SAUTI CHRISTIAN CARDON)

Cardon ameongeza kuwa pia wameaini hali ya usalama imezorota zaidi katika miezi miwili iliyopita kwenye jimbo la Kandahar na nchi nzima jambo ambalo linachangia zaidi shughuli za ICRC kuweza kuwafikia waathirika wengi.