Skip to main content

Fedha zitolewe kusaidia matibabu ya nasuri (Fistula):Ban

Fedha zitolewe kusaidia matibabu ya nasuri (Fistula):Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuchangishwa kwa takriban dola milioni 750 zitakazo gharamia matibabu kwa akina mama milioni 3.5 wanaosumbuliwa na maradhi ya uzazi ya nasuri au obstetric fistula itimiapo mwaka 2015.

Kwenye ripoti yake kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Ban ametoa wito wa kuwekezwa fedha zaidi kwenye matibabu ya ugonjwa huu ikiwemo upasuaji ili kuwandolea akina mama tatizo la ugonjwa huu unaowasumbua. Hata kama ugonjwa huu umeangamizwa kwenye nchi zilizostawi bado unaendelea kuwasumbua akina mama na wasichana kwenye nchi zinazoendelea wengi wanaoishi katika sehemu za vijijini.

Ban anasema kuwa ugonjwa wa nasuri unaweza kuzuiwa ikiwa akina akina mama watapata huduma za uzazi zifaazo. Shirika la afya duniani WHO linakadiria kuwa kati ya akina mama 50,000 na 100,000 kote duniani waanaathirika na ugonjwa huu kila mwaka idadi ambayo Ban anaitaja kuwa ndogo kwa kuwa wengi wa akina mama kutoka vijijini wanaoathirika na ugonjwa huu hawafiki hospitalini.