UM umetoa wito wa amani katika duru ya pili ya uchaguzi Guinea

30 Septemba 2010

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa viongozi wa Gunea kuhakikisha kwamba duru ya pili ya uchaguzi wa Rais inafanyika kwa amani katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

Wawakilishi wa mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi wametoa wito huo kufuatia hofu kwamba uchaguzi huo Guinea unaweza kusababisha matatizo ya kiusalama katika kanda nzima kama hautofanyika kwa amani.

Duru ya pili ya uchaguzi wa Rais iliahirishwa hadi Oktoba 10 baada ya kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo kusema nchi yake haiko tayari kufanya uchaguzi huo. Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchi humo amerejea jukumu la Umoja wa Mataifa la kusaidia uchaguzi huo ili uwe huru, wazi na wa mani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter