Ripoti ya utafiti wa kilimo cha kasumba nchini Afghanistan imeonyesha kuwa uzalishaji wa zao hilo umepungua kwa kiasi kikubwa.
(YURY FEDETOV)
Ripoti hiyo ya utafiti iliyotolewa leo inasema kilimo bado kinaendelea katika maeneo machache ya majimbo ya Kusini na magharibi mwa Afghanistan, maeneo ambayo yameghubikwa na wanamgambo na mitandao ya uhalifu. Ripoti inasema kilimo hicho kimepungua kutoka ekari 193,000 mwaka2007 hadi ekari 123,000 mwaka huu, na majimbo mawili makubwa kwa usalishaji ni Helmand na Kandahari.
Tani 3600 pekee ndio zilizopatikana mwaka huu ikiwa ni pungufu ya asilimia 48. Sababu kubwa imetajwa kuwa ni ugonjwa ulioathiri kilimo hicho Helmand na Kandahar, lakini pia kushuka kwa bei ya zao hilo kwenye soko la kimataifa jambo ambalo limewafanya wakulima wengi kufikiria kuliacha.