Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufukua makaburi Nepal kutasaidia kupatikana haki na ukweli:UM

Kufukua makaburi Nepal kutasaidia kupatikana haki na ukweli:UM

Umoja wa Mataifa umepongeza hatua iliyochukuliwa na mamlaka ya Nepale ambayo inafukua miili ya wanafunzi watano waliozikwa wakati nchi hiyo ilipotumbukia kwenye mzozo wa kiasa miaka kadhaa iliyopita ili kufanya uchunguzi zaidi kubaini namna mauwaji yao yalivyoendeshwa.

Umoja wa Mataifa imesema kuwa kitendo hicho ambacho imekiita cha kusaka ukweli wa mambo, kitasaidia siyo tu kuwaleta kwenye mkondo wa haki wale wote waliohusika lakini pia ni ishara njema ya kuzingatiwa haki inatendeka.

Wanafunzi hao watano ni miongoni mwa maelfu ya wananchi waliopoteza maisha wakati nchi hiyo hiyo ilipotumbukia kwenye mzozo wa kisiasi mwaka 2006. Inadaia kuwa watu zaidi ya 1,300 walipoteza maisha yao kabla ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani yaliyomaliza mzozo huo.

Zoezi la ufukuaji wa maiti hizo kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi linaongozwa na maafisa wa Kamishna ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, wakisaidiana na maafisa wengine kutokaka Kikosi cha Polisi cha Nepal, na wataalamu wengine wa kimataifa wa mambo ya kale.