Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yashirikiana na mashirika ya kiraia kuwanikisha matumizi ya simu kwa wakimbizi ili kuunganishwa na familia zao

UN yashirikiana na mashirika ya kiraia kuwanikisha matumizi ya simu kwa wakimbizi ili kuunganishwa na familia zao

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi limeanzisha mradi wa majaribi nchini Uganda, ambao unawapa fursa wakimbizi kuanza kutambuana na kuwasiliana na familia zao kwa kutumia mawasiliano ya simu za mikononi.

Mwakilishi wa UNHCR nchini Uganda Kai Nielsen amekaribisha hatua hiyo na kuongeza kuwa ukurasa mpya sasa umefunguka kwani sasa wakimbizi wanaweza kuwasiliana tena na jamaa zao popote duniani. Waratibu wa mpango huo wanakusudia kuusambaza mradi huo katika nchi nyingine kama hatua hii ya majaribio itafanikiwa