Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala kuhusu maisha ya watu wa asili kabila la Batwa nchini Burundi

Makala kuhusu maisha ya watu wa asili kabila la Batwa nchini Burundi

Umoja wa Mataifa umeendelea na juhudi zake za kuhakikisha kila jamii duniani inapata haki sawa na wengine.

Katika siku ya kimataifa ya watu wa asili mapema mwezi huu wa Agosti Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alitoa wito kwa nchi zote duniani kuzingatia sheria za kimataifa na kuwapa haki sawa watu wa jamii za kiasili kwa kuwashirikisha kwenye mchakato wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Nchini Burundi kuna makabila makubwa matatu, Wahutu, Watutsi na Batwa ambao ni watu wa asili. Batwa wamekuwa wakilalamika kuwa wametengwa kwa muda mrefu na sasa umewadia wakati wa kujumishwa katika masuala mbalimbali ya jamii,jambo ambalo serikali ya Buirundi imeanza kulifanyika kazi kama alivyobaini mwandishi wetu Ramadhan Kibuga katika makala hii.