Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Virusi vya mafua ya H1N1 sio tishio tena kwa dunia:WHO

Virusi vya mafua ya H1N1 sio tishio tena kwa dunia:WHO

Kamati ya dharura ya shirika la afya duniani WHO imesema dunia haiko tena katika daraja la sita la kiwango cha hatari ya mafua ya H1N1.

Imesema hivi sasa dunia inaingia katika kipindi cha baada ya madhara. Mtazamo huo umetolewa baada ya kamati kuwa na mkutano kwa njia ya simu leo na pia tathimini ya hali ya kimataifa na ripoti kutoka nchi mbalimbali ambazo zinasema wanachokipata sasa ni mafua ya kawaida.

Hata hivyo kamati hiyo imesema kuingia kipindi cha baada ya madhara hakumaanishi kwamba virusi vya H1N1 ndio vimetoweka moja kwa moja kama anavyofafanua mkurugenzi mkuu wa WHO Bi Margaret Chan

(SAUTI YA MARGARET CHAN)

Ameongeza kuwa pamoja na hivyo kimataifa kiwango cha maambukizi ya H1N1 ni kidogo sana ukilinganisha na wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo na maambukizi ya wakati ambao sio msimu wa mafua hajaarifiwa kabisa kutoka upande wowote.