Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visiwa vya Pacific vimeathirika zaidi na unene wa kupindukia:WHO

Visiwa vya Pacific vimeathirika zaidi na unene wa kupindukia:WHO

Utafiti wa shirika la afya duniani WHO umebaini kwamba katika nchi kumi za visiwa vya Pacific zaidi ya asilimia 50 ya watu wameathirika na unene wa kupindunia .

Maeneo yaliyoathirika zaidio kwa mujibu wa utafiti huo ni American Samoa ambayo ni sehemu ya Marekani ambako asilimia 80 ya wanawake wana unene wa kupindukia huku kisiwa cha Fiji kikiwa na zaidi ya asilimia 30 ya walio na uzito wa kupita kiasi. Dr Temo K Waqanivalu mtaalamu wa lishe na shughuli za viungo wa ofisi ya WHO inayowakilisha Pacific Kusini mjini Suva Fiji amesema kwa kiasi Fulani analamu lishe duni kwa matatizo hayo ya kiafya kwenye visiwa vya Pacific.

Ameongeza kuwa kiwango cha watu wanaokula vuyakula vya asili kimepungua sana kwani hakiwezi kushindana na vyakula vinavyoingizwa toka nje ambavyo vingi ni vya makopo na vilivyotengenezwa viwandani.