Skip to main content

Adhabu kali inadidimiza vita dhidi ya ukiwmi kwa wapenzi wa jinsia moja:UM

Adhabu kali inadidimiza vita dhidi ya ukiwmi kwa wapenzi wa jinsia moja:UM

Ripoti mpya ya shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP inasema kuendelea kufanya kuwa ni kosa la jinai ngono ya wanaume kwa wanaume eneo la Asia Pacific kunasababisha udhalilishaji na ukiukaji wa haki za binadamu jambo ambalo linarudisha nyuma mapambano dhidi ya ukimwi.

Kati ya nchi 48 za eneo hilo nchi 19 zikiwemo Afghanistan, Bhutan, Kiribati na Malaysia zina sheria inayopinga baina ya wanaume kwa wanaume , sheria mbazo mara nyingi zinatumika kwa njia ambayo ni ya unyanyasaji na ukiuaji wa haki za binadamu. Ripoti hiyo mpya inasema kwamba polisi wanawalenga wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao na watu ambao wamebadili jinsia zao, ambapo huwadhalilisha, kuwatesa na kuwaweka mahabusu katika baadhi ya nchi hizo kwa kisingizo cha kutekeleza mazingira ya sheria.

Ripoti hiyo inasema polisi pia kuwasumbua wafanyakazi wanaochagiza mapambano ya ukimwi ambapo wengine ni wapenzi wa jinsia moja au waliobadili jinsia inaingilia vita dhidi ya ukimwi. Karibu nusu ya nchi za Asia Pacific wanaume ambao ni wapenzi wa jinsia moja wako katika hatari kubwa ya kupata virusi vya HIV.