Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapiganaji wa Darfur kusalimisha silaha kwa hiyari

Wapiganaji wa Darfur kusalimisha silaha kwa hiyari

Zaidi ya wapiganajia wa zamani 800 walioshiriki mapigano katika eneo la magharibi mwa Sudan, Darfur wanatarajiwa kushiriki kwa shughuli ya wiki tatu ya kuwasilisha silaha zao kwa hiyari katika hatua ambayo inasaidiwa na operesheni ya pamoja ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika eneo la Darfur, UNAMID

Japo shughuli ya kuwapokonya silaha wapiganaji hao ni programu ya serikali ya Sudan, UNAMID inasaidia kwa kupeana msaada ya usafiri, ulinzi na ushauri kuhusiana na ukimwi.

Programu hiyo ambayo ilianzishwa kama programu ya makubaliano ya amani na Darfur inapeana msaada wa kifedha kwa wapiganaji hao ili wajisalimishe huku serikali ikipeana fedha ya awali ambapo itafuatwa na misaada mengine.