Skip to main content

UM umezindua mwongozo kuzuia ukatili kwa wanawake maeneo ya vita

UM umezindua mwongozo kuzuia ukatili kwa wanawake maeneo ya vita

Umoja wa Mataifa umezindua mwongozo maalum wa kuzuia ukatili wa kijinsia ukiwemo ubakaji kwa Wanawake waliopo kwenye maoneo ya vita.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya ukatili wa kijinsia kwenye maenmeo ya migogoro, Margot Wallstrom, amekieleza kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa kuwa mwongozo huo una taarifa sahihi za namna ya kuzuia ukatili huo kwa wanawake.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakitumia mbinu mbali mbali za kuweza kuzuia  ukatili wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro, ikiwemo kuwasindikiza wanawake katika maeneo ya mahitaji muhimu kama kuchota maji, kutafuta kuni na mashambani.