Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ameteua jopo la kumshauri kuhusu haki za binadamu nchini Sri Lanka

Ban ameteua jopo la kumshauri kuhusu haki za binadamu nchini Sri Lanka

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo ameteua jopo la wataalamu kumshauri kuhusu masuala ya madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na sheria wakati wa hatua za mwisho za mgogoro wa Sri Lanka uliomalizika mwaka jana.

Amesema wajumbe hao watatu watamshauri kuhusu utekelezaji wa kutimiza haki za binadamu ahadi iliyowekwa na Katibu Mkuu na Rais wa wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa baada ya Ban kuzuru nchi hiyo Mai mwaka jana. Muindonesia Marzuki Darusman atakuwa mwenyekiti wa jopo hilo na wengine wawili ni Mwafrika Kusini Yasmin Sooka na Steven Ratner wa hapa Marekani. Jopo hilo linatarajiwa kukamilisha jukumu lake miezi minne tangu walipoanza kazi yao.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ban iliyotolewa na msemaji wake, jopo hilo litaangalia mbinu za, viwango vya kimataifa, na uzoefu katika mchakato mzima kwa kuzingatia aina na ukubwa wa madai ya ukiukaji nchini Sri Lanka. Na itakuwa wazi pia kwa serikali ya nchi hiyo endapo itataka kuhusisha wataalamu wake.