Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa Haki za Binadamu wametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa Aung San Suu Kyi

Wataalamu wa Haki za Binadamu wametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa Aung San Suu Kyi

Serikali ya Myanmar imetakiwa kuzingatia wito wa kitengo cha kujitegemea cha haki za binadamu cha Umoja wa Mataifa na kumuachia mara moja mwanaharakati na mwanasias Daw Aung San Suu Kyi.

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya mahabusu na vizuizi kilipitisha azimio kumuhusu Daw Aung San Suu Kyi, ambalo limewekwa bayana hadharani.

Katika taarifa iliyotolewa leo mtaalamu anayeangalia mambo ya haki za binadamu nchini Myanmar Tomas Ojea Quintana amesema kwamba kama katika maoni yao matano yaliyopita kundi hilo limebaini kwamba kuendelea kumunyima uhuru Daw Aung San Suu Kyi ni kinyume cha sheria na ni jambo lisilo kubalika.

Ameongeza kuwa kundi hilo limeiomba serikali ya Myanmar kutekeleza mapendekezo ya kundi hilo ya siku za nyuma ili Myanmar iweze kukidhi sheria na misingi ya kimataifa ya haki za binadamu.