Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wa ngazi za juu wa mkutano wa UM unatafuta njia za kuzuia tishio la uhalifu

Mjadala wa ngazi za juu wa mkutano wa UM unatafuta njia za kuzuia tishio la uhalifu

Uhalifu wa kupangwa katika baadhi ya maeneo sasa umekuwa ni tishio kubwa la usalama wa kimataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameuambia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba wakati tishio hilo likiongezeka ndivyo suala hilo linavyopewa umuhimu katikia ajenda za kimatataifa.

Ameongeza kuwa njia muafaka ya kukabiliana na uhalifu huo wa kupangwa iko bayana, nayo ni mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya uhalifu na ametatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzingatia hatua kubwa ya kuadhimisha mwaka wa kumi wa mkataba wa Palermo kwa kuongeza juhudi za kimataifa za kukabiliana na uhalifu huo.