Skip to main content

Katibu Mkuu wa UM azuru mataifa ya Afrika

Katibu Mkuu wa UM azuru mataifa ya Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezuru mataifa matatu ya Afrika, Burundi, Cameroon na Afrika ya Kusini ambako mbali na kukutana na viongozi wa nchi amekuwa akipigia upatu malengo ya milenia.

Alipokuwa Burundi ameipongeza nchi hiyo kwa kudumisha amani baada ya vita vya muda mrefu na mchango wake wa walinda amani nchini Somalia. Ameitembelea Burundi ikiwa katika mchakato wa uchaguzi na wakuu wa jeshi la Burundi nao wametumia fursa hiyo kufikisha kero zao za ukosefu wa uwezo katika kikosi cha AMISOM nchini Somalia. Kutoka Bujumbura Ramadhani Kibuga anaarifu.