Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwathirika wa mateso ya vita katika JKK azungumzia maafa aliopata na msaada anaotoa kihali kwa waathirika wengine

Mwathirika wa mateso ya vita katika JKK azungumzia maafa aliopata na msaada anaotoa kihali kwa waathirika wengine

Mnamo mwanzo wa mwezi Septemba UM uliwakilisha ripoti mbili muhimu, zilizochapishwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu na pia kutoka Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC).

Baada ya kufanyika uchunguzi kamili, ripoti hizi mbili zilithibitisha kwamba inayumkinika makosa ya vita yalitendeka katika eneo la mashariki la JKK. Kadhalika utafiti huoulionyesha makosa ya jinai dhidi ya utu wa raia yalifanyika kwenye eneo hili la mashariki, vitendo vilivyodaiwa kuendelezwa na vikosi vya Serikali pamoja na majeshi ya mgambo.

Hivi karibuni, mtayarishaji wa vipindi vya Kifaransa wa Redio ya UM, Jean-Pierre Ramazani alizuru eneo la mashariki katika JKK, na alipata fursa ya kufanya mahojiano na baadhi ya watu walioathirika na ukiukaji wa haki za kiutu ulioelezewa kwenye ripoti za Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu pamoja na MONUC. Alipokuwepo huko alirikodi mazungumzo maalumu na mwathirika mmoja wa mateso ya watu wenye silaha, anayeitwa Yvonne Kisali, mkaazi wa Jimbo la Kivu Kusini katika eneo la Muami wa Itombwe. Yvonne ni Raisi wa Jumuiya ya Wathirika wa Vita au Victims de Guerre. Hapa inafaa kuhadharisha wasikilizaji wetu kwamba Jean-Pierre Ramazani, anayehoji na Yvonne Kisali, mhojiwa wanazungumza Kiswahili kwa lahaja ya kikongamano.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.