Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zimechagizwa kujitolea vikosi,ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani

Nchi zimechagizwa kujitolea vikosi,ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya walizi wa mani Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amezishukuru nchi mbalimbali na wananchi wake kwa kujitolea.

Siku ya walinda amani ilitengwa maalumu kwa ajili ya kuwaenzi na kuwakumbuka waliopoteza maisha katika mipango ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani katika sehemu mbalimbali duniani.

Mmoja wa wafanyakazi wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID vilivyoko Darfur Sudan ni Emmanuel Mollel na amezungumza nami akizichagiza nchi kujitolea vikosi, maisha ya walinda amani na umuhimu wa siku hii.