Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amelaani shambulio dhidi ya kituo cha michezo cha UNRWA Gaza

Ban amelaani shambulio dhidi ya kituo cha michezo cha UNRWA Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mashambulio na uharibifu uliofanywa na wavamizi kwenye vituo vya michezo ya watoto vya mpango wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi kwa Wapalestina UNRWA.

Michezo maalumu ya kiangazo inayoandaliwa na UNRWA hutoa fursa kwa watoto kuburudika na kupumzika kidogo na hali ngumu na maisha ya dhiki ya kila siku Ukanda wa Gaza. Ban ameutaka uongozi wa Gaza kuhakikisha usalama kwa shughuli za Umoja wa Mataifa na kuruhusu UNRWA kufanya kazi zake bila pingamizi zozote.

Ripoti ya UNRWA imesema watu 30 waliokuwa na silaha na kuvaa vinyago usoni walishambulia na kuwasha moto moja ya majengo ya michezo ya UNRWA kwenye ufukwe wa Gaza.