Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Honduras kukabiliana na mauaji ya waandishi wa habari

UM waitaka Honduras kukabiliana na mauaji ya waandishi wa habari

Baadhi ya kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameisihi serikali ya Hondorous kuchukua hatua mara moja ya kusitisha dhulma dhidi ya waandishi wa habari.

Nchini humo katika muda wa wiki sita, wafanyi kazi saba wa vyombo vya habari katika taifa hilo la Merekani ya Kati wameuwa, huku wengine wengi wakitishiwa maisha. Wataalamu hao wamesema wanahimiza serikali kuchukua hatua zote kuchunguza vifo na vitisho hivyo, pamoja na kuwahukumu waliohusika ili kuwalinda waandishi wa habari.

Hususani wanaitaka serikali kuunda tume huru ili kumilika hali hii na kutafuta hatua zitakazochukuliwa ili kuwalinda waandishi wa habari vyema na kuzui hali kama hiyo kutotokea tena katika siku za usoni.