Skip to main content

Juhudi mpya zinahitajika kutokomeza mifumo mibaya ya ajira kwa watoto

Juhudi mpya zinahitajika kutokomeza mifumo mibaya ya ajira kwa watoto

Wawakilishi zaidi ya 450 kutoka nchi 80 wanakutana The Hague Uholanzi kujadili sulala la ajira kwa watoto.

Wawakilishi hao wametoa wito wa kuwepo na juhudi mpya za kimataifa kutokomeza mifumo mibaya zaidi ya ajira kwa watoto ifikapo mwaka 2016. Wito huo umetolewa wakati dalili zinaonyesha kuwa mapambano dhidi ya ajira kwa watoto yanapoteza kasi yake.

Mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa na serikali ya Uholanzi kwa ushirikino na shirika la kazi duniani ILO pia utajadili hatua zilizopigwa tangu kuridhiwa kwa mkataba wa ajira mbaya kwa watoto wa ILO namba 182 mwaka 1999.

Pia utaangalia njia muafaka ya kuhakikisha malengo ya kutokomeza mifumo hiyo ya ajira mbaya yanatimia ifikapo mwaka 2016. Constance Thomas ni mkurugenzi wa programu ya kimataifa ya kutokomoza ajira ya watoto ILO