Baraza la usalama limezitaka nchi kulivalia njgua suala la uharamia

28 Aprili 2010

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka nchi zote kuliingiza suala la uharamia katika sheria zake za makosa ya jinai.

Wito huo upo katika azimio lililowasilishwa na shirikisho la Urusi na kupitishwa na wote jana Jumanne. Baraza hilo pia limemuomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoa taarifa ndani ya miezi mitatu ya njia zitakazowezekana kufanikisha lengo la kuwashitaki na kuwafunga watu wanaohusika na vitendo vya uharamia na uporaji wa kutumia silaha katika bahari ya hindi kwenye pwani ya Somalia.

Balozi wa Uganda kwenye Umoja wa Mataifa Ruhakana Rugunda amelikaribisha azimio hilo akisisitiza kwamba uharamia ni tatizo la kimataifa ambalo linatoa changamoto kwa nchio zote.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter