Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetoa tahadhari kutokana na kuzuka ugonjwa wa sotoka Asia

UM umetoa tahadhari kutokana na kuzuka ugonjwa wa sotoka Asia

Ugonjwa wa sotoka unaoathiri midomo na miguu kwa wanyama umezuka katika nchi za Asia za Japan na Jamuhuri ya Korea ambazo awali zilitangaza rasmi kuwa hazina tena ugonjwa huo.

Mlipuko wa ugonjwa huo umelifanya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kutoa wit oleo wa kimataifa wa kuchukua tahadhari.

Ogonjwa wa sotoka mara nyingi huathiri wanaya wenye kwato kama ng'ombe, kondoo, mbuzi na nguruwe, na husababisha homa kali na wanaya hao kuvimba na kubabuka midomo na miguu. Ugonjwa huu hauathiri binadamu.