Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili wa kimapenzi bado ni tatizo kubwa linalohitaji suluhu haraka

Ukatili wa kimapenzi bado ni tatizo kubwa linalohitaji suluhu haraka

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu katika masuala ya ukatili wa kimapenzi kwenye migogoro Margot Wallström, ameliarifu baraza la usalama juu ya juhudi zake za kushinikiza suala la ukatili wa kimapenzi kuendelea kupewa uzito na hatua za kuuzuia kupewa kipaumbele.

Ameonya kuwa ubakaji unaochagizwa na masuala ya kisiasa ni tatizo linalosumbua kwa sasa na limeshuhudiwa katika ghasia za baada ya uchaguzi Kenya na hivi karibuni kabisa katika mitaa ya Guinea. Uhalifu huo amesema unaleta matatizo ya kiusalama yanayohitaji hatua za kiusalama kuyatatua.

Pia amekaribisha hatua ya kupanua wigo wa kuyaaibisha makundi ya wahalifu wanaowaingiza watoto jeshini, na amesema kuamua kujumuisha makundi yanayoshukiwa kuendeleaza vitendo vya ubakaji na dhuluma za kimapenzi ni kitendo cha kupongezwa.