Skip to main content

Mpango wa kulinda amani Darfur umepokea polisi wa kike kutoka Ghana

Mpango wa kulinda amani Darfur umepokea polisi wa kike kutoka Ghana

Mpanmgo wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID umepokea polisi wa kike 50 kutoka Ghana mwishoni mwa wiki.

Kuwasili kwa wanawake hao kunaifanya idadi ya wanawake polisi wa UNAMID kutoka Ghana kufikia 110 .Ghana ni moja ya nchi iliyona mchango mkubwa wa polisi kwwenye mpango huo wa UNAMID.

Wakati huohuo mwakilishi maalumu wa UNAMID Ibrahim Gambari amekuwa na mazungumzo na Rais al Bashir kuhusu walinda amani wanne wa UNAMID waliotekwa hivi karibuni ambao sasa wameachiliwa huru.