Skip to main content

Al Bashir ndiye mshindi wa uchaguzi wa kihistoria wa vyama vingi Sudan

Al Bashir ndiye mshindi wa uchaguzi wa kihistoria wa vyama vingi Sudan

Tume ya uchaguzi nchini Sudan imetangaza matokeo ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi baada ya miaka 24.

Rais wa sasa Omar al Bashir ambaye ametolewa kibali cha kukamatwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC ametangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo. Salva Kiir aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la Sudan Kusini SPLM ametangazwa mshindi na kama Rais wa serikali ya Kusini ambayo kwa kiasi Fulani ina madaraka ya uongozi.

Uchaguzi katika sehemu zote nchini Sudan ulighubikwa na malalamiko ya kuwepo kwa udanganyifu na vitisho kwa wagombea huku wasimamizi wa kimataifa wakisema viwango vya kuchaguzi huo havijafikia hadhi inayohitajika.