Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani

Leo ni siku ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani

Leo ni siku ya kimataifa ya ya ugonjwa wa kifua kikuu, inayoadhimishwa kila mwaka kote duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, msemaji wa mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria Michel Kazatchkine amesema kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya kifua kikuu na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo itawezekana endapo jitihada zitakwenda sambamba na malengo yaliyowekwa hivi karibuni jambo ambalo litasaidia pia kukabiliana na tiso la dawa mchanganyiko kutofanya kazi ipasavyo.

Ameongeza kuwa uamuzi ambao utachukuliwa na viongozi mwaka huu utakuwa muhimu saana kuendeleza mapambano yaliyopo na kutimiza malengo ya milenia .