Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF imeipa msaada wa vifaa vya shule Jamuhuri ya Afrika ya Kati

UNICEF imeipa msaada wa vifaa vya shule Jamuhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati limekabidhi vitabu vya hesaabu elfu 60,vya Kifaransa elfu 60 na vya muongozo wa walimu elfu mbili na mia nne kwa wizara ya elimu, elimu ya juu na kitengo cha utafiti.

Mfumo wa elimu Jamuhuri ya afrika ya Kati kwa mwaka 2008 wavulana waliokuwa shuleni ni aslimia 56 na wasichana asilimia 49. Na idadi ya watoto wanaoacha shule ni kubwa hususani kwa wasichana ambapo ni asilimia 54.

Ukosefu wa vitabu umechangia saana kuwa na kiwango kidogo cha elimu, kwani vitabu viwili vinatumika kwa kila wanafunzi tisa. Mradi huu unasaidia maeneo mbalimbali yanayokabiliwa na migogoro ya vita, na wanafunzi takribani 145,000 watanufaika na mradi huo.