Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misri yatetea hali ya tahadhari iliyodumua kwa miaka 30

Misri yatetea hali ya tahadhari iliyodumua kwa miaka 30

Serikali ya Misri imetetea hali ya tahadhari iliyotangazwa nchini humo mwaka 1981 baada ya mauaji ya Rais Anwar Sadat.

Katika taarifa yake kwenye baraza la haki za binadamu leo Dr Sihab amesema hali hiyo ya hatari imekuwepo katika hatua za kukabiliana na ugaidi.

Amesema kumekuwepo na matukio mengi ya mauaji ya viongozi kadhaa wa kisiasa na , na nchi hiyo imeshuhudia vitendo vya kigaidi dhidi ya wageni na ongezeko la chuki za kidini. Amesema hali hiyo ya tahadhari itaondolewa pindi sheria mpya ya kukabiliana na ugaidi itakapopitishwa.